
Marafiki wawili John na Jeremy walikwenda kuomba kazi katika kampuni Fulani,
Kwa habari nzuri wote wakapata kazi na kuianza,
Walifurahia kazi hiyo na kuona malengo yao yatatimia ndani ya muda mfupi,
Hali walizokuwa nazo kabla hazitajirudia Tena,
Baada ya kufanya kazi kwa takribani miezi mitatu Jeremy alipandishwa cheo ya bosi ya kampuni hiyo,
John Ali huzika sana,
Alijisemea hivi “Tumeajiriwa wote lakini anampandisha yeye cheo na Mimi anipandishi”
Manun’guniko yake yalipozidi Alaina Ni Bora aende kwa bosi kumuuliza,
Bosi huyu alikuwa ni mwelewa na alikuwa na hekima,
Akamwita Jeremy wakawa wote ofisini,
Watatu Yani John, Jeremy na Bosi.
Kisha bosi akamwambia John “Nenda Sokoni kaulize Bei ya matikiti”
John akaondoka,
Huyooo Sokoni,
Baada ya muda mfupi akarudi,
Ndipo akaulizwa “Ni Bei gani?”
Akajibu “Matikiti Ni Tsh. 3,000/=”
” Sawa bosi akasema”
Kisha akamwambia Jeremy aende naye sokoni kuuliza Bei ya matikiti,
Jeremy alichukua muda kidogo kurudi,
Alipofika jibu hivi,
“Matikiti yapo ya Elfu tatu, Elfu Tano na Elfu sita…
Bei za matikiti zinatofautiana kutokana na uzito wa tikiti na ubora wake,
Matikiti ya elfu sita ambayo Ni mazuri yanakaribia kuisha,
Muuziaji amesema atatupunguzia Bei ikiwa tutawahi Sasa hivi…. “
Jeremy akamaliza kujibu,
Mwishoni bosi akamuuliza John,
” Umeona mwenzako alivyojibu? Wote si mlienda Sokoni?”
Hatimaye John alielewa Ni kwa Nini Jeremy alipandishwa cheo,
Ya kwamba Jeremy alifanya zaidi ya alichoagizwa,
Wote wakaondoka ofisini wakiwa na amani,
Sasa nimetumia stori hii kwa sababu Nataka kukwambia sheria hii,
Ni sheria ya *Sababu na Athari *
Wazungu wanaiita *Cause and Effect*
Sheria hii ilianzia kutoka kwa mwanafalsafa Nguli “Aristotle”
Sheria inasema hivi…
“Kila Jambo linatokea kwa sababu, Na kila Athari Kuna sababu Fulani”
Katika Biblia sheria hii pia inaitwa Sheria ya Kupanda na Kuvuna,
” Utavuna ulichopanda”
Kama ilivyokuwa kwa John yaweza kuwa kwako pia,
Unajiuliza Ni kwanini unakwama?
Kwanini Kuna baadhi ya malengo hauyafikii?
Na wakati Fulani unafikiria kuwa umelogwa?
Hapana,
Ila Huenda sababu ipo hapa,
Unalengo kubwa sawa…
•Matendo Madogo Madogo unayofanya sio ya kukufanya ufikie Lengo lako,
•Aina ya watu ulio nao karibu Ni wale wanaokuridisha nyuma Bila ya wewe kujua,
•Hauna watu maalumu ambao unataka kujifunza kutoka kwao,
n.k
Sababu zaweza kuwa nyingi,
Jiulize swali Hili kwa kila unalofanya,
“Je hili ninalofanya sasa litanisaidia kufikia Lengo langu?”
Na uzuri wa sheria hii Ni kwamba,
Waweza badilisha Mambo leo,
Ambayo yatakufanya ufikie hatma yako,
Fikiria Sasa kwa Nini unakwama?
Lazima Kuna sababu fulani,
Unapoanza wiki hii fahamu sababu zinazokufanya ubaki hapo hapo Bila kufikia Lengo lako,
Umejifunza kitu hapa?
Umeelewa?
Usisite kunitumia Ujumbe,
Mpaka Wakati mwingine,
@ Ishi Njozi Media.
Leave a comment