
“Mdomo wako utakuponza”
Unaelewa Nini unapoambiwa msemo huo?
Leo nitakwambia kosa ambalo wenye Njozi (Ndoto kubwa) wengi hufanya,
Na hatimaye kuchelewa Kutimiza Njozi zao au hata Kutotimiza kabisa,
Haya hebu tuanze,
Karibu kila mtu amepewa mdomo,
Lakini sio kwamba kila wakati na kila sehemu ukiwa na kila mtu unatakiwa kuongea,
Yaani Kufungua mdomo wako…e
Kwa sababu,
Unapokuwa mtu wa kutojua wapi uongee, kwa Nani uongee, na nini uongee waweza pata hasara hizi,
•Kuzuia nafasi yako ya kujifunza zaidi kutoka kwa huyo mtu,
Tambua hili wanaojua Mambo mengi Mara zote hawapendi kusema Sana,
Unapokuwa unaongea Sana wao waweza kaa kimya au kubaki Wanasema,
“Enhee”,
“Ilikuwaje?”
“Wachawe!!!”
Na wewe unasema hapa ndipo kumbe yote unayosema yeye anajua,
Ila kwa sababu anapenda kujifunza zaidi ndo maana anakusikiliza,
Na pia kwa kuwa mtu wa kuongea tu,
•Upo hatarini kusema mipango yako kwa watu ambao wanaweza kutumia Kama Silaha dhidi yako,
Unao marafiki, ndugu na jamaa…
Kila mtu ana fikra zake, Mipango yake, na utofauti wake,
Lakini “Kila mtu anataka kuwa na Mafanikio makubwa maishani”
Hivyo unapokuwa na NJOZI kubwa na Ni mtu wa kusema Sana,
Waweza sema Njozi Yako kwa watu ambao wakishatoka hapo kuondoka na kupambana mpaka watimize kabla yako,
“Usiseme Seme”
“Tulia”
Ninakunong’oneza maneno haya kwa sababu Asilimia tisini na Saba hawajui Hili,
Ngoja Ni kuaminishe zaidi,
Watu Hawa,
1.Albert Eisten,
2.Jk.Lowling,
3. Elon Musk,
4. Michael Jordan,
5. Warren Buffet,
Na wengine wengi wote Ni watu ambao sio waongeaji Sana,
Waweza angalia Mafanikio ya kila mmoja Google,
Huu ni ujumbe ambao utasikia Mara chache unaongelewa,
Hivyo Basi chukua hatua Sasa,
Badilika Sasa,
Kwa sababu Huenda asikukumbushe mtu mwingine yeyote,
Ikiwa somo hili limekugusa toa maoni yako
@ Ishi Njozi Media.
What’s Up No. 0683506299
Leave a comment