
Katika kila nyanja ya maisha Kuna malengo fulani yanawekwa na matarijio fulani yanakuwepo.
Bila hata wewe katika maisha yako unatamani kufanya jambo Fulani lakini umekuwa unashindwa ufanyaje ili ufanikiwe.

Leo nimekuandalia makala hii uweze kujua Mambo matatu ambayo waweza kufanya hata Sasa na kuanza kuona mabadiliko.Karibu.
1.Badilisha Viwango Vyako.
Viwango ni kipimo cha mafanikio katika nyanja fulani. Yaweza kuwa katika Masomo, michezo n.k.Hata katika Mambo binafsi.
Ni muhimu kubadilisha Viwango ulivyonavyo katika maisha yako kwa sababu, hauwezi kufanya vizuri zaidi ya viwango ulivyojiwekea.

Taa wakati wa usiku ina umuhimu wa kuhakikisha tunaondokana na giza na kujua wapi unaelekea na hivyo kutopotea unapotembea njiani.
Vivyo hivyo viwango unavyotaka katima maisha yako Ni vipi. Kutambua kiurahisi ni fanya haya mambo mawili ni muhimu kuyafanya kwa kuandika
- Andika Mambo yote ambayo hautayavumilia Tena katika maisha yako.
- Andika Mambo ambayo unatamani kuhakikisha u ayafikia kwa nguvu zako zote.
Baada ya kufanya zoezi hilo kwa uaminifu hatimaye utapata kuwa na viwango vyako kamili katika maisha yako.
Andika yote unayohitaji katika maisha yako hata Kama kwa sasa siyo Kama unavyopenda mambo yawe.
Baada ya kukamilisha hatua ya Pili ambayo ni,
2.Badilisha Imani potofu zinazo kurudisha nyuma.
Asilimia tisini na Saba ya watu wanajua sababu kwamba kitu fulani hatiwezi kufanya kazi.Yaani kufahamu kuwa mambo fulani hayawezekani.
Hivi unajua shida ni kwamba Imani potofu ndizo zinazofanya wawe natazamo huo na hata wewe waweza kuwa miongoni kama ukiwa na Imani potofu.
Sasa Ni muhimu kujitathmini Ni mmbo gani ambayo unaamini na kwa namna moja au nyingine ya akuzuia kuhakikisha unafikia malengo yako katika maisha.
“Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo…”
Waebrania 11:1
Kumbuka kuwa pamoja na watu wenye Imani potofu kuhusu mafanikio au maisha hata Wewe hatimaye utakuwa Kama wao hivyo chukua tahadhari.
Ikiwa utabadilisha Viwango vyako , na unakuwa na Kuondoa Imani zinazojurudisha nyuma, hatimaye itabidi kubadilisha mbinu au namna ya ufanyaji mambo ambayo ni hatua ya tatu.
3.Badilisha Mbinu
Kufanya Jambo Fulani kwa mbinu moja huku ukitarajia matokeo tofauti ni Ujinga.
Hivyo badala ya kurudia kufanya mambo kwa njia hiyo hiyo Ni vema kuhikisha tafuta mbinu bora upate matokeo tofauti na ya juu Zaidi.
Waweza kufikia lolote unalohotaji ikiwa tu utakuwa tayari kuyatende kazi hayo uliyojifunza hapo juu.Kun
Ikiwa unatamani kuwa katika group la WhatsApp upate matumaini kila siku bonyeza link hii https://wa.me/message/3CFBDK5NVWUEF1
Mpaka wakati mwingine kwa heri.
Leave a comment