
Mhandisi amekamilisha kutengeneza injini na anatoa Sheria ambazo lazima zifuatwe.

Nini kitatokea iwapo kanuni hizo hazitafuatwa bila shaka injini itakufa na kuharibika kabisa.
Hata katika maisha yako ikiwa hautafuata sheria maalumu kuhusu Ndoto zako hautafanikiwa.

Zifuatazo Ni sheria nne ambazo Ni muhimu kufahamu ili uweze kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yako.
1.Sheria ya Imani (Law Of Belief)
Sheria hii inasema hivi
“Kila unalo liamini kwa hisia , Hilo huwa uhalisia wako”
Yaani Imani yako katika Jambo lolote unalofanya au unalotarajia kufanya italeta matokeo.
Ikiwa unaamini unaweza kufanikiwa na kuwa katika Hali bora kiuchumi unaweza.
Hili pia linahusika katika nyanja zingine pia za maisha. Wakati fulani Yesu alimwambia mwanamke aliyekuwa anatokwa damu “Imani yako imekuponya”
Yaani Ukiwa unaamini utaweza utaweza tu. Hivyo kanuni ya kwanza ni “Imani thabiti kwa kila unalotaka”
2.Sheria ya matarajio (Law of expectation).

Sheria hii inasema hivi,
“Kila unalotarajia kwa ujasiri huwa unabii wa kujitimizia mwenyewe”
Sasa ikiwa unatarajia kuwa na mafanikio makubwa na Hali kubwa ya kiuchumi utaweza tu.
Katika nyanja zote hilo linahusika matarajio katika kila kitu yataleta matokeo Kulingana nayo.
Hivyo Basi kuwa na matarajio ya kushinda na kufanya vizuri tu katika maisha yako na utapata Kama ulivyotarajia.
Hata asubuhi inashauriwa kusema “Naamini jambo fulani zuri kitatokea katika siku yangu ya leo”
Kumbuka hata Kama unapitia hali ngumu kiasi gani bado kunakitu Cha kujifunza kutoka katika Hali hiyo.
3.Kanuni ya kuvutia (Law of attraction).

Sheria hii inasema hivi,
“Wewe ni sumaku inayoishi”
Yaani kupitia mawazo yako unaweza kuvutia kitu chochote kwako.Tunashauriwa kuwa na fikra sahihi.
Ukiwa na mawazo hasi katika kila jambo hautaweza kufanikisha Jambo lolote,kuwa na mtazamo sahihi na chanya katika maisha yako.
Yaani maisha yako ni matokeo ya mawazo yako yaani fikra kuhusu maisha. Kuwa na mtazamo chanya na utaweza kufanya makubwa.
Amua Leo ondoa wazo lolote ambalo linakufanya uwe na mtazamo hasi kuhusu maisha yako na kuwa na mawazo chanya tu.Jaribu hata kwa siku kumi bila kufikira mawazo hasi.
4.Sheria ya mawasiliano kati ya Ulimwengu wa ndani na wa nje
Sheria hii ipo hivi,
“Uzoefu wa kile kilichopo nje hudhihirisha nini kilichopo ndani”
Yaani kile kilichopo ndani yako lazima kitaonekana tu nje. Hivyo Basi tabia yako ya ndani au mafanikio yako yataoneshwa tu kwa Hali yako ya nje
Hivyo basi hakikisha kile unalolifanya ndani yako Ni sahihi, huenda isiwe kivitendo lakini kupitia maneno yako. Kwa sababu kila lililopo ndani hatimaye litadhihirika.
Haijalishi Ni kitu gani ambacho unakihitaji bado unaweza kufikia iwapk hautakuwa na mawazo hasi katika Ulimwengu wa ndani.
Kati ya mpinduzi makubwa katika kizazj hiki Ni kwamab kwa kubadilisha mitizamo ya ndani (Ulimwengu wa ndani ) utaweza kubadilisha kila kitu katika maisha yako.
Sasa ni wakati wa kusimamia maisha yako na kuamua kuongozwa na kanuni sahihi, na Kaa ukijua zaidi ya wasilimia Sabini na tano ya kil utakayekutana hafuati Sheria hizi.
Unaweza kuleta mabadiliko ukiamua. Ikiwa unatamani kuwa katika group la what’s up la bure upate Nguvu ya kupigania njozi kila siku bonyeza link hii https://wa.me/message/3CFBDK5NVWUEF1https://wa.me/message/3CFBDK5NVWUEF1
Mpaka wakati mwingine kwahari.
Leave a comment