Maadui Wakubwa Wawili…

Hivi unajua kuwa woga na Ujinga ndiyo maadui wakubwa katika kufikia njozi yako?

Mwanafalsafa mmoja amewahi kusema kati ya eneo lenye utajiri mkubwa duniani ni makaburini.

Yaani kujua watafanyeje kushinda Ni kwa sababu kwa walishindwa kuwashinda maadui hawa wawili.

Sasa Hawa ndio maadui wakubwa wawili wa Njozi yako.

1.Woga.

Hivi Ni hisia gani unazipata pale ambapo unatakiwa kufanya Jambo fulani jipya?

Au kufanya jambo fulani ambalo wengi hawaamini kuwa inawezekana?

Sasa sikia,

Woga Mara zote hufanya Mambo yaonekane kuwa makubwa wakati Ni madogo au kuona hayawezekani wakati yanawezakana.

Haijalishi ni njozi gani ambayo umejiwekea inawezekana kufikia ikiwa utaondoa hofu au woga.

Ikiwa utashinda woga au hofu utakuwa katika njia ya kufikia Njozi yako.

Adui wa pili ni huyu,

2.Ujinga.

Ujinga ni Hali ya kutokuwa na Maarifa fulani.

Haiwezekani kujua kila kitu na hivyo tutabaki kuwa wajinga tu ndo maana tunashauriwa kujifunza kila siku kitu kipya.

Ujinga ninao usema hapa ni ule wakutojua unanjozi gani na unataka kufanya Nini maishani.

Yaani unaishi tu bila yakujua unataka kufanya Nini katika maisha yako.Kuna Mambo ma

Kuna mambo mawili kukataa UJINGA au ubaki hapo hapo na uongeza utajiri kaburini.

Sikutishii ila ninacho kuhamasisha Ni kukataa UJINGA.

Jinsi ya kuwashinda maadui hao

1.Pata Maarifa.

Kubali kujifunza, usiwe kama Ni mtu ambaye hautaki kubadilika na unataka kubaki hapo hapo tu.

Yaani pale unapojitoa kupata maarifa mapya hatimaye utaweza kusonga mbele zaidi.

Kati ya maarifa muhimu kufahamu Ni Wewe Ni Nani na utawezaje kuwakikisha unakuwa Wewe halisi.

Ikiwa utaamua kupata maarifa hatimaye utapata hili,

2.Hamu (Nia thabiti)

Unapo pata Maarifa kamili kuhusu jambo fulani hatimaye utapata NIA THABITI ya kupambania Njozi yako.

Hofu au woga ambao ulikuwa nao hautakuwepo Tena na utafikia Njozi yako.

Nashukuru kwa kusoma makala hii mpaka Sasa. Kusoma mpaka sasa hakuna faida yoyote ikiwa hautachukua hatua.

HIVYO CHUKUA HATUA UFIKIE NJOZI YAKO.

Ikiwa unatamani kuwa katika group la What’s up liitwalo Ishi Njozi.

Bonyeza link hii ili uweze kujua zaidi https://wa.me/message/3CFBDK5NVWUEF1

Kwa heri mpaka wakati mwingine,Najali furaha yako.Kwa Jeri.

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started